Serikali za Tanzania na Burundi kwa kushirikina na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhgulika na masuala ya wakimbizi UNHCR limetangaza kufuta rasmi hadhi ya ukimbizi kwa wakimbizi wa Burundi katika kambi za Nyarugusu na Nduta mkoani kigoma Ifikapo June mwakani.
Mkurugenzi idara ya wakimbizi wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania Soodi Mwakibasi amesema uamuzi huo ni matokeo ya makubaliano ya pande tatu hizo baada ya kubaini kuendela kusua sua kwa wakimbizi hao kurejea nchini mwao kuanzia mwaka 2017 licha kuwa nchi yao ya Burundi kutokuwa katika tatizo lolote la kiuslama kauli ambayo pia imeungwa mkono na Mkuu wa mkoa wa kigoma Saimon Sirro, balozi wa mdogo wa Burundi nchini Kengwa jeremia na pia msemaji toka shirika la kuhudumia wakimbizi
Wakimbizi wapatao 103 717 toka nchini Burundi wanahifadhiriwa katika kambi za Nyarugusu na Nduta mkoani kigoma
#StarTvUpdate