Mkurugenzi wa huduma za udhibiti mbolea kutoka TFRA Happines Mbele amesema TFRA Imepeleka tani 63,228 za mbolea katika wilaya ya…Mkurugenzi wa huduma za udhibiti mbolea kutoka TFRA Happines Mbele amesema TFRA Imepeleka tani 63,228 za mbolea katika wilaya ya…

Mkurugenzi wa huduma za udhibiti mbolea kutoka TFRA Happines Mbele amesema TFRA Imepeleka tani 63,228 za mbolea katika wilaya ya mbinga kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa saba, zikiwa na thamani ya bil.21.8 ili kuwasaidia wakulima wa wilaya hiyo katika msimu mpya wa kilimo 2025-26.

Amewataka wakulima kuendelea kupima afya ya udongo ili kuweza kutumia mbolea sahihi kulingana na uhitaji wa zao lakini pia amewahimiza kujisajili kwenye mfumo wa pembejeo za ruzuku ili kuondoa usumbufu pindi wanapohitaji pembejeo hiyo kwa shughuli zao.

Mkulima Ernest Komba wakijiji cha Utili amekiri kuwa matumizi mabaya ya mbolea yanaleta athari kwenye kilimo kwa kushusha uzalishaji na vilevile kuharibu afya ya udongo.

Amewashauri wakulima kuzingatia mafunzo yaliyotolewa na wataalam wa kilimo na kufuata ushauri wa maafisa ugani walioajiriwa na serikali kwa kazi hiyo ili shughuli za kilimo wanazozifanya ziwe na tija na kuwaongezea kipato.

Na, @dkhan1410
@RFAOnline
@Habaristartv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *