#HABARI: Mpaka sasa baadhi ya wanachama wa Yanga hawajafanikiwa kuvuka mpaka wa Tanzania na Malawi – Kasumulu kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za uhalali wa hati ya chanjo ya manjano na baadhi ya madereva kutofanikiwa kukamilisha mchakato hati za kusafiria za muda.
Uongozi umeendelea kupambania wanachama kufanikiwa kuvuka kwa sababu kilomita zaidi ya 600 kutoka Kasumulu mpaka kufika Lilongwe ambapo inaweza kuchukua zaidi ya saa 11.
Pamoja na changamoto hizo bado wanachama wameendelea kuamini wataenda kuwaunga mkono timu yao inayotarajia kucheza mchezo wa kwanza wa rauandi ya pili Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers F.C.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.