Wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likitangaza kamati yake mpya marefa, hakuna Mtanzania aliyepata fursa ya uteuzi kwenye kamati hiyo nyeti.

Wajumbe 14 wameteuliwa katika kamati hiyo mpya wakitka katika kanda tofauti za soka zilizo chini ya CAF lakini Tanzania imefungiwa vioo.

Kamati hiyo ambayo itahudumu kwa miaka minne ijayo, itakuwa chini ya Rais, Olivier Kabene Safari kutoka DR Congo na Makamu wa Rais aliyeteuliwa ni Victor Gomes kutoka Afrika Kusini.

Kundi la wajumbe 12 wa kamati hiyo linajumuisha waliowahi kuwa marefa maarufu barani Afrika ambao wengi hivi sasa ni wakufunzi katika nchi mbalimbali.

Wajumbe hao na nchi zao kwenye mabano ni Ali Tomusange (Uganda), Lidya Tafessa (Ethiopia), Inacio Candido (Angola), Janny Sikazwe (Zambia), Fatou Gaye (Senegal) na Lemghaifry Bouchaab (Mauritania).

Wengine ni Sinko Zeli (Ivory Coast), Irabor Uwugiaren (Nigeria), Hadq Yahya (Morocco), Djamel Haimoudi (Algeria), Rene Louzaya (Congo) na Menkouande Evariste wa Cameroon.

Kamati hiyo ina majukumu 18 ya msingi yaliyo kwenye orodha hapo chini

-Kusimamia kozi za waamuzi waandamizi

-Kusimamia kozi za wakufunzi na watathmini wa waamuzi waandamizi

-Kusimamia kozi za uhuishaji (Refresher Courses)

-Kufuatilia na kurudisha mrejesho wa refa mmojammoja kwa Vyama Wanachama wa CAF juu ya viwango vyao kwa mashindano yote yaliyo chini ya CAF.

-Uandaaji wa zana za kufundishia kwa marefa, wakufunzi na watathmini.

-Uandaaji wa Program za maendeleo.

-Uandaaji wa program za ufanyaji kazi kwa kanda

-Kuteua marefa wa mashindano tofauti ya CAF.

-Kufuatilia ufanisi wa wakufunzi, watathmini na marefa

-Kufuatilia na kusaidia maendeleo ya marefa kwa vyama wanachama.

-Kujaza data za marefa na kupanga madaraja ya marefa.

-Kutunza mawasiliano ya marefa na taarifa zao binafsi.

-Kutunza ripoti za utimamu wa marefa.

-Kuanzisha ubunifu wa kiteknolojia

-Kutoa usaidizi kwa wataalam wa tehama

-Kupanga akademia ya marefa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *