
Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace wanapanga kumuuza mlinzi wa Uingereza Marc Guehi mwezi Januari na Liverpool haiko tena mstari wa mbele kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, huku Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich wakimtaka. (The I paper)
Kiungo wa kati wa England na Crystal Palace Adam Wharton, 21, ndiye analengwa na Manchester United kwa uhamisho wa Januari, ingawa anaweza kugharimu takriban £70m. (Team talk)
Liverpool na Chelsea zote zilikataliwa na Everton msimu wa joto baada ya kuonesha nia yao ya kumnunua mlinzi wa kati wa England Jarrad Branthwaite, 23. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham na Liverpool wote wanamtaka winga wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 25. (Talksport)
Inter Milan wamekanusha tetesi kuwa wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Brazil Neymar, 33, mwezi Januari, baada ya mkataba wake kuisha Santos. (Corriere dello Sport)
Mkufunzi wa Manchester United Ruben Amorim anavutiwa sana na beki wa kushoto wa Inter Milan Federico Dimarco, 27, lakini mchezaji huyo ana nia ya kusalia San Siro kwa sasa. (Tuttosport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sunderland haitaonesha tena nia yake ya kumnunua beki wa Bologna na Colombia Jhon Lucumi katika dirisha dogo la usajili la Januari baada ya ofa ya pauni milioni 24 kukataliwa kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu wa joto. (Sky Sports)
Mlinda lango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen bado hajafanya uamuzi wa iwapo atasalia katika klabu hiyo mwezi Januari, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 33 akitaka kucheza kabla ya Kombe la Dunia msimu ujao. (Florian Plettenberg)
Juventus wana nia ya kumrejesha kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali kwenye Serie A lakini Newcastle wamedhamiria kumshikilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wamekubali kulipa pauni 350,000 pamoja na bonasi muhimu kwa Barnsley kwa Josh Kenchington, 15, akiwapiku Manchester United, Tottenham na Brighton kwenye saini ya beki huyo wa chini ya miaka 15 wa England. (Sky Sports)
RB Leipzig wameweka bei ya euro 100m (£87m) kwa winga wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 18 Yan Diomande. (Sky Germany)
Wolves haitarajiwi kufanya usajili wowote mkubwa mwezi Januari na kuna uwezekano wa kuwafuata wachezaji wao muhimu, akiwemo kiungo wa kati wa Brazil Andre, 24, ambaye alilengwa na Juventus msimu uliopita. (Mail)