
Wimbi la chuki dhidi ya utawala haramu wa Israel limeongezeka katika maeneo mbalimbali duniani sambamba na kupungua himaya na uungaji mkono kwa utawala huo nchini Marekani.
Ripoti zinaonyesha kuwa, katika wakati ambao uungaji mkono wa umma kwa utawala wa Israel nchini Marekani umepungua kwa kiasi kikubwa na wasiwasi ndani ya jamii ya Wayahudi wa nchi hiyo umeongezeka, mitaa ya Barcelona nchini Uhispania imekuwa uwanja wa maandamano makubwa dhidi ya Israel. Tangu kuanza hujuma za kinyama za Israel katika Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, majimbo na vyuo vikuu vingi vya Marekani vimekuwa uwanja wa maandamano dhidi ya jinai za utawala huo ghasibu na mauaji ya watoto wachanga.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na Washington Post, unaonyesha kuwa, 42% ya Wayahudi wa Marekani wanajizuia kuonyesha utambulisho wao hadharani.
Wakati huo huo, uchunguzi wa maoni ya New York Times unaonyesha kuwa uungaji mkono kwa Israel umepungua kutoka asilimia 47 hadi 34, huku uungaji mkono kwa Wapalestina ukiongezeka kutoka asilimia 20 hadi 35.
Asilimia 40 ya Wamarekani wanaamini kuwa Israel inalenga raia kwa makusudi. Huko Ulaya, maelfu ya waandamanaji mjini Barcelona, Uhispania, walifunga barabara kuu na kukabilia na polisi kwa ajili kuandamana dhidi ya “mauaji ya halaiki huko Gaza.” Matukio haya yanaonesha kuwa, madai ya hivi karibuni ya Israel kuhusu usitishaji vita yameshindwa kupunguza hasira inayoongezeka duniani kulaani vitendo vya utawala huo ghasibu.