
Chanzo cha picha, Getty Images
-
- Author, Simon Stone
- Nafasi, Manchester United reporter
Ruben Amorim anatazamia kurejea kwa ligi kuu ya soka nchini England kwa matarajio makubwa kwa Man Utd.
Lakini mechi nne kubwa zinawasubiri United kuanzia kwa Liverpool.
Huenda zikabadili msimamo wao kwa njia nzuri au mbaya.
Kikosi cha Amorim kilionesha mchezo mzuri zaidi msimu huu kilipoishinda Sunderland 2-0 kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Matokeo hayo yalipunguza shinikizo lililokuwa limeanza kuongezeka kwa kocha huyo Mreno hasa baada ya kupokea kichapo dhidi ya Brentford ugenini wiki moja kabla ya hapo.
Tangu hapo, mmilikialiye na hisa chache Sir Jim Ratcliffe ameunga mkono Amorim, akigusia kuwa huenda ikachukua miaka mitatu kwa kocha huyo wa zamani wa Sporting kuanza kubadilisha matokeo ya Old Trafford – na vilevile akiwakumbusha mashabiki kuwa ilimchukua Sir Alex Fergusin muda mrefu kubadilisha matokeo wakati alipojiunga na timu hiyo 1986.
Hata hivyo, Amorim anajua ni wachache mno watakaoamini maneno ya Ratcliffe ikiwa timu itakosa kupiga hatua muhimu kuboresha nafasi ya 15 waliyomaliza msimu uliopita ambayo yalikuwa matokeo mabaya zaidi kwao tangu 1973-74 ambapo walishushwa daraja.
Ushindi dhidi ya Sunderland umeupandisha hadi nafasi ya kumi, mara ya pili pekee msimu huu ambapo wamemaliza mechi na kuingia ndani ya kumi bora katika jedwali la EPL.
Ilikuwa ushindi wao wa kumi ndani ya mechi 34 tangu Amorim alipochukua mikoba ya Eric ten Hag mwezi Novemba mwaka jana. Ingawa hawajashinda mechi mbili mfululizo.
United hawangekuwa na kibarua kigumu zaidi Jumapili kuliko Liverpool uwanjani Anfield, mahali ambapo hawajashinda tangu 2016 ma hadi msimu uliopita wamefunga bao moja pekee katika mechi nane.
Ni wachache mno wanaodhani kuwa United watarejea kutoka Merseyside na alama tatu.
Kulingana na matarajio, ni mechi zinazofuata ambazo zitakuwa ngumu zaidi brighton nyumbani, Nottingham Forest na Tottenham Ugenini.
Kinadharia, nafasi nzuri ya kuzoa alama na kupanda kwenye jedwali hadi katika nafasi za kufuzu michuano ya bara Ulaya.
Katika chumba cha kubadilisha jezi na chumba cha viongozi wa timu hili ndilo linalopewa kipaumbele msimu huu na dhihirisho kuwa kuna hatua iliyopigwa.
Hata hivyo, katika misimu miwili iliyopita United wamepoteza nyumbani dhidi ya Brighton na ugenini dhidi ya Nottingham Forest na Tottenham.
Msimu uliopita Amorim alikuwa anaiongoza United katika mechi zote hizo.
Inayofuata ni ratiba ya mechi za Man Utd na vile vile kuangazia matokeo ya 2024-25, pamoja na tathmini ya Amorim ya baada ya mechi na mashabiki.
Ni bora kukisia kuwa matokeo bora yanatariwa wakati huu.
Oktoba 19: Liverpool ugenini (2024-25: 2-2 tarehe 5 Januari)
Inayotarajiwa kuwa mechi ngumu zaidi kati ya nne zijazo za Man utd ndio mechi pekee ambayo wamezoa alama katika misimu miwili iliyopita. Mwezi Januari, Lisandro Martinez aliiweka Utd kifua mbele – mara ya kwanza hilo lilitokea ugani Anfield tangu Wayne Rooney alipofunga bao la kipekee 2016 – lakini Amad Diallo akasawazisha kuwapa alama moja, kisha Harry Maguira akapoteza nafasi nzuri ya kuwapa ushindi katika dakika za mwisho.
” iko wazi kabisa,” alisema Amorim wakati huo.
”Tukimakinika, huwa tunapigania kila mpira, tukiumia na wakati tunapochoka na mechi imeisha huwa timu nzuri. Iwapo hatutafanya hivyo kila wakati tutapoteza mechi nyingi.
Shabiki David aligonga ndipo katika tathmini yake ya baada ya mechi kwenye makala ya BBC aliposema: ‘Hatimaye, Man utd ya ukweli imejitokeza.
Je, tutaendelea hivyo? natumai ningekuwa na ujasiri kuhusu jawabu kuwa ndio!
Oktoba 25: Brighton, nyumbani (2024-25: 1-3 tarehe 19 Januari)
Mchana uliokuwa mbaya ulizidishwa na kauli kali ya Amorim baada ya mechi.
Hivi sasa Brighton wameshinda mechi tatu mfululizo Old Trafford na hii ilikuwa mbaya zaidi.
Baada ya kupatikana katika shambulizi la kushtukiza, United walisawazisha kupitia penalti iliyofungwa na Bruno Fernandes na wakaponea baada ya bao la wapinzani wao kukataliwa na VAR,
Lakini Kaoru Mitomaakapenyeza mpira nyuma ya Noussair Mazraoui na kuwarejesha Brighton uongozini tena kabla ya mlinda lango Andre Onana kuruhusu mkwaju wa kawaida wa chini kutoka kwa Yasin Ayari kumpita mikononi mwake bila shinikizo lolote na kumpatia nafasi rahisi Georginio Rutter kufunga.
”Katika mechi kumi za mwisho za ligi ya Uingereza tumeshinda mbili” alisema Amorim. Wazia hii ni nini kwa shabiki wa Manchester United. Hebu fikiria hii ni nini kwangu. Tunapata kocha mpya ambaye anapoteza zaidi ya kocha aliyekuwa kabla yake. Nina ufahamu kamili wa hilo. Sisi ni timu mbaya zaidi labda katika historia ya Manchester United.”
Mfuasi Su hakutaka kuangazia makosa ya Onana kuhusu uamuzi wa mashabiki wa BBC Sport, akisema: “Brighton walikuwa na lengo tangu dakika ya kwanza, United hawakuwa. Kuzungumza kuhusu makosa ya Onana kutafunika tu matatizo mengi Old Trafford.”
Novemba mosi: Nottingham Forest, ugenini (2024-25: 0-1 on 1 Aprili)
Losing at the City Ground in the Premier League for the second successive season was bad enough for Manchester United. That Anthony Elanga should score the winner just twisted the knife deeper.
Kupoteza katika uwanja wa City Ground mara ya pili mfululizo ilikuwa jambo baya zaidi kwa Man Utd.
Hasa ikizingatiwa kwamba Anthony Elanga ndiye aliyefunga bao la ushindi inazidi kutonesha kidonda.
United walimuuza Elanga kwa klabu ya Nottingham Forest kwa pauni milioni 15 mwaka 2023 kwakuwa Erik ten Hag hakukubaliana na maoni ya Ralf Rangnick kuhusu uzuri wa mshambuliji huyo wa Uswidi.
Bao la Elanga lilikuwa zuri alipokimbia na mpira uwanjani yadi 50 baada ya Forest kuondoa hatariya mpira wa kona kutoka kwa Man utd huku Mazraoui akirejea nyuma kabla ya kupiga mkwaju wa chini hadi kwenye neti.
” Ni badiliko moja kutoka kwa mpira wa kona”, anasema Amorim.”Hatuwezi adhibiwa na bao aina hii”.
Adam alikuwa akipambanua katika kipindi cha spoti cha BBC akisema:”Nachukia ikikaa kama rekodi iliyovunjwa, lakini Ruben Amorim alikosea kwa mara nyingine tena.Utengenezaji wa fomu duni, chaguo mbovu za kikosi cha kwanza, mabadiliko duni na kutoweza kubadilika. Anajichimbia kaburi lake mapema sana.”
8 Novemba: Tottenham, Ugenini (2024-25: 0-1 tarehe 16 Februari)
Kipigo cha kudhalilisha cha Manchester United chini ya uongozi wa Amorim kufikia sasa kilikuwa katika fainali ya Europa mwezi Mei maana iliwakosesha nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu.
Lakini kupoteza dhidi ya Tottenham ilionekana jambo lililozoeleka msimu uliopita – ilitokea mara nne ikiwemo ushindi kwenye kombe la EFL.
Mwezi Februari Spurs iliandikisha historia ya kuwa timu ya kwanza kuishinda Man Utd mara tatu ndani ya msimu mmoja tangu Chelsea mwaka 2012-13.
James Maddison alifunga bao la pekee katika mechi ya ligi mjini London baada ya dakika 13.
Spurs aidha walikuwa wakikamilisha ushindi wa nyumbani na ugenini dhidi ya United kwa mara ya kwanza tangu 1989-90, wakati ambapo Terry Venables alikuwa mkufunzi.
“Tofauti katika mechi ni kwamba walifunga na sisi tukashindwa kufunga,” Amorim anasema.
Maoni ya Peter katika jukwa la spoti la BBC ilikua zaidi ya kulaani: “Hakuna maono, hakuna malengo, hakuna juhudi.”
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Ambia Hirsi