
Mahmoud Reza Aghamiri, Rais wa Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti na mmoja wa wahusika wakuu katika mradi wa nyuklia wa Iran, amesema kuwa nchi yake ina uwezo kamili wa kutengeneza bomu la nyuklia, lakini haijachukua hatua hiyo kutokana na msimamo wa kidini wa Kiongozi Mkuu, Ayatollah Ali Khamenei.
Hata hivyo, alionya kuwa fatwa hiyo inaweza kubadilika.
Katika mahojiano yaliyorushwa jioni ya Jumatano kupitia tovuti ya “Adventure and its Visual Media”, Aghamiri alizungumzia kwa kina hali ya mvutano kati ya Iran na Israel katika vita vya siku 12, pamoja na hasara iliyopatikana, ikiwemo kuuawa kwa wataalamu wake sita wa nyuklia.
Katika mahojiano yaliyorushwa jioni ya Jumatano kupitia tovuti ya “Adventure and its Visual Media”, Aghamiri alizungumzia kwa kina hali ya mvutano kati ya Iran na Israel katika vita vya siku 12, pamoja na hasara iliyopatikana, ikiwemo kuuawa kwa wataalamu wake sita wa nyuklia.
Aghamiri ambaye Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inamtaja kuwa mwanasayansi wa nyuklia alisisitiza kuwa ikiwa Iran itaamua kutengeneza silaha za nyuklia, basi inaweza kufanya hivyo kwa ustadi mkubwa.
“Sehemu muhimu zaidi ya kazi hiyo ni urutubishaji wa madini ya nyuklia,” alieleza.
Alipoulizwa kama wanasayansi wa nyuklia wa Iran waliwahi kufikiria juu ya kutengeneza silaha hizo, alijibu wazi, “Bila shaka. Wazo hilo liliwahi kuwapo akilini mwao. Lakini fatwa ya Kiongozi Mkuu ilizuia jambo hilo.”
“Bila shaka. Wazo hilo liliwahi kuwapo akilini mwangu hasa kama mwanasayansi. Lakini fatwa ya Kiongozi Mkuu ilizuia jambo hilo.”
Javad Mogoui, katika sehemu moja ya mahojiano yake, anarejelea “gharama kubwa” ambayo Iran imelipa kwa ajili ya kurutubisha madini, na Mahmoudreza Aghamiri anajibu kwa kusema kuwa tu kuwa na teknolojia ya nyuklia ni “kizuizi” ka maadui na kwamba kuwa na “uwezo” wa kutengeneza silaha hizo kunaweza kutosha kuzuia shambulio.
Fatwa inayozuia silaha za nyuklia yaweza kubadilika
Ayatollah Ali Khamenei amekuwa akisisitiza kwamba Iran haina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia, akieleza kuwa matumizi ya silaha hizo ni haramu kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu. Mnamo Februari 20, 2009, alinukuliwa akisema:
“Hatuamini katika mabomu ya atomiki. Hatuna silaha hizo, wala hatutazifuatilia. Dini yetu inakataza matumizi ya silaha za maangamizi. Hizi ni silaha za kuharibu ardhi na kizazi jambo ambalo kitabu kitakatifu cha kiislamu Qur’an imelipiga marufuku.”
Hata hivyo, Aghamiri alieleza kuwa licha ya fatwa hiyo, kuna uwezekano wa mabadiliko:
“Kama nilivyosema awali, yeye ni mujtahid. Anaweza kubadilisha fatwa au maoni yake wakati wowote.”
Aliongeza kwa maneno ya mafumbo:
“Kama wao watagonga chini ya meza, nasi tutagonga chini ya meza pia. Lakini kwa sasa, tunafanya kazi yetu ya kitaalamu.”
Utunzaji wa nyenzo za nyuklia na mafunzo ya kitaaluma
Katika sehemu ya hotuba yake, Mahmoud Reza Aghamiri anasema, bila maelezo, kwamba kuhifadhi “vifaa vyenye joto ni vigumu moto” ni vigumu zaidi kuliko kuhifadhi bomu la nyuklia lililotengenezwa, akiongeza: “Hivyo ni kweli kwa mafuta ya roketi.
Alisisitiza kuwa huwezi kumfundisha mwanafunzi taaluma ya nyuklia bila kumfundisha pia misingi ya kutengeneza bomu, na kusema:
“Iwapo nchi itahitaji, basi kila kitu kinawezekana.”
Kwa mara nyingine alitetea msimamo wa Iran kuwa teknolojia ya nyuklia ni haki ya wananchi wa Iran, akikumbusha kuwa kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, kulikuwapo mpango wa kujenga vinu vitano vya nyuklia, lakini mpango huo haukutekelezwa baada ya mapinduzi asema Agha Miri.
Mauaji ya maprofesa wa vyuo vikuu yalikuwa “ya kuumiza sana”

Chanzo cha picha, Tasnimnews
Aghamiri aliita mauaji ya maprofesa na wataalamu wa nyuklia wa Iran kuwa “madhara makubwa sana”, lakini akasema kuwa wataalamu wa Shirika la Nguvu za Atomiki la Iran hawakulengwa moja kwa moja.
“Tuna ujuzi wa kutosha wa kujenga upya kile kilichoharibiwa.”
Ingawa hakuthibitisha madai ya Marekani kuwa vituo vya nyuklia kama Fordow viliharibiwa na mashambulizi, alitoa changamoto:
“Kama kweli wamemaliza kila kitu, kwa nini hawataki kuachana na suala hilo?”
Alikosoa pia juhudi za baadhi ya wanaharakati waliowataka viongozi wa Iran kusitisha urutubishaji wa madini ya nyuklia, akisema:
“Huo ni mchezo wa maadui.”
Usiku wa jinamizi: Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran

Chanzo cha picha, Morteza Nikoubazl/NurPhoto via Getty Images
Aghamiri alisimulia tukio la usiku wa Juni 13, siku ya kwanza ya mashambulizi ya Israel dhidi ya maeneo ya Iran, ambapo wataalamu sita wa idara ya fizikia ya nyuklia katika Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti waliuawa.
Aliambiwa na mamlaka za usalama kufuta safari aliyokuwa amepanga kuelekea kwenye hosteli ya chuo karibu na mji wa Savadkouh.
“Ilikuwa taraehe 13 mwezi Juni nilishtuka saa tisa usiku kwa sauti ya king’ora za ulinzi. Simu yangu ikaita, nikaambiwa nitoke haraka nyumbani.”
Alipakizwa gari aina ya Pride, si la usalama bali kutoka kwa mtu mwingine. Wakiwa njiani, walipokea taarifa kuwa Ahmad Reza Zolfaghari, mtaalamu mwenzake, alikuwa amevamiwa.
Walipofika kwenye eneo hilo, walikuta pia gari la zimamoto mbele ya nyumba ya Abdolhamid Minouchehr, mwingine kati ya waliouawa.
Aghamiri alisema walinzi walimpokonya simu na kumpeleka mahali pasipojulikana:
“Sikujua nilikuwa wapi, na familia yangu haikujua pia. Ilikuwa kama jinamizi.”
Alisema pia alipokea taarifa za awali zisizothibitishwa kuhusu kuuawa kwa Fereydoun Abbasi Davani, aliyewahi kuongoza Shirika la Atomiki la Iran. Mwanzoni ilisemekana kuwa ni mke wake aliyeuawa, lakini baadaye ikathibitishwa kuwa mwili wake ulikuwa umesukumwa hadi kwa jirani kwa nguvu ya mlipuko.
Abbasi alikuwa ametegwa pia mwaka 2010 katika shambulizi la pamoja lililomuua Majid Shahriari, lakini yeye akaokoka wakati huo.
Shabaha ya Israel: Chuo Kikuu karibu na Gereza la Evin
Licha ya mazingira magumu, Aghamiri alisema aliendelea kwenda chuoni kila siku kwa saa moja.
Alisimulia kuwa siku ya mwisho ya vita, wakati Gereza la Evin lilipolengwa, yeye na wenzake walikuwa kwenye Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti, ambacho kiko karibu na gereza hilo.
“Tulihisi kuwa lengo la Israel lilikuwa jengo la Idara ya Fizikia ya Nyuklia, hivyo tulilifunga na kulihamisha.”
Katika siku hizo 12 za vita, Iran ilitangaza kuwa wataalamu 11 wa nyuklia waliuawa hii ni kwa mujibu wa maafisa wa Iran,
Uvujaji wa taarifa na ujasusi wa ndani
Mauaji ya wataalamu na makamanda wa juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (IRGC) yalizua mjadala mkubwa kuhusu kiwango kikubwa cha uvujaji wa taarifa na ujasusi wa maadui ndani ya Iran, ambacho kilitajwa kuchangia kudhoofika kwa uwezo wa Iran kujibu mashambulizi hayo.
Mara baada ya kumalizika kwa vita hivyo vya siku 12, serikali ya Iran iliwahukumu kifo watu kadhaa waliotuhumiwa kwa ushirikiano na Israel.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid