#HABARI: Wakati taifa likielekea katika uchaguzi mkuu, wa kuwachagua viongozi mbalimbali akiwemo Rais, Wabunge na Madiwani, Taasisi ya mwanamke na nguvu ya kijani nchini, imeandaa kongamano la viongozi wa dini, wafanyabiashara vijana na taasisi mbalimbali lengo likiwa kuhamasisha amani.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es saalam, kuhusu Kongamano hilo linalotarajia kufanyika oktoba 25 hadi 27 2025, katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini dar es saalam, mwenyekiti wa taasisi ya mwanamke na nguvu ya kijani dkt judith mhina spendi, amesema kama mfanyabiashara ni jukumu lake katika kuhimiza amani nchini. Huku akisisitiza kwamba uwepo wa amani ni muhimu katika maendeleo ya taifa lolote lile duniani.
Kwa upande wake Rais wa mitume na manabii nchini Martine Shaboka, amesema kila mtanzania atambue anajukumu la kulinda amani nchini.
•Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania