Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Lindi limeendesha semina maalum kwa viongozi wake kutoka kata zote za wilaya hiyo, ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo juu ya taratibu sahihi za upigaji kura na umuhimu wa ushiriki wao katika mchakato wa uchaguzi.
Semina hiyo ya siku moja imefanyika leo katika Manispaa ya Lindi, chini ya uongozi wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Said Mushangani ambaye amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi wanashiriki uchaguzi kwa amani, umoja na nidhamu, ili kuhakikisha demokrasia inaendelea kustawi nchini.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi