Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe amezielekeza hospitali zote nchini kuhakikisha zinatoa huduma zote za dharura kwa wagonjwa bila kuchelewesha na bila kuangalia uwezo wa kifedha kwa wakati huo.

Dkt. Shekalaghe ametoa maelekezo hayo mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo ya kujenga uwezo wa utoaji huduma za dharura kwa wagonjwa wa ajali na kiharusi kwa hospitali za rufaa za mikoa awamu ya kwanza, akisisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya kwa haraka na bila ubaguzi wa kifedha.

#AzamTVUpdates
✍Theresia Mwanga
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *