Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Matari Masige amesema wanaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya miundombinu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 383 mkoani humo itakayoongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi .

Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa barabara ya njia nne yenye urefu kwa kilometa 29 kutoka Uyole hadi Ifisi kwa shilingi bilioni 138.7, barabara za Ibanda–Kiwira Port na Kajunjumele–Itungi Port (km 32) kwa shilingi biilioni 38.3, na jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa shilingi bilioni 14.1.

Miradi mingine ni kituo cha huduma ya pamoja mpakani Kasumulu/Songwe kinachogharimu shilingi bilioni 26.4 na ujenzi wa barabara ya Katumba–Mbambo–Tukuyu yenye urefu wa kilometa 83 kwa shilingi bilioni 86.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *