Haya yanafanyika huku muda wa kumchagua waziri mkuu mpya ukisonga.

Nchi hiyo ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa wiki iliopita baada ya chama cha Komeito, mshirika mdogo wa chama cha LDP kujiondoa kwenye muungano tawala baada ya miaka 26.

Na sasa kiongozi mpya wa LDP Sanae Takaichi amekutana na mwenzake wa chama cha Japan Innovation party, JIP, Alhamis katika hatua ya kutafuta washirika wapya.

Iwapo kutakuwa na muungano kati ya chama cha LDP na JIP basi hilo huenda likafungua njia ya Takaichi kuchaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Japan.

Takaichi anahitaji wingi wa viti 233 ili ateuliwe na bunge kama waziri mkuu ila chama chake cha LDP kina viti 196 tu bungeni. Chama cha JIP kina viti 35 na hiyo inamaanisha kuwa bado atakosa viti viwili.

Kwa upande mwengine vyama vyengine vitatu vya upinzani ambavyo viko katika mazungumzo ya kumpata mgombea wa pamoja wa waziri mkuu vina jumla ya viti 210. Vyama hivyo pia katika mkutano wao wa Jumatano vilibaini ya kuwa bado kuna kutoelewana baina yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *