Shamra shamra za kampeni za siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, wagombewa hususan wale wa Urais wamekuwa wakitembea katika maeneo ya mbalimbali ya nchi kunadi sera na ahadi, miongoni mwa ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa karibu na wagombea wote 16 ni kuhusiana na sekta ya afya. Doyo Hassan Doyo- ni mgombea Urais wa NLD

“Watu wote wanajipimia wao wenyewe, akijisikia maumivu akijinyoosha dukani Paracetamol Nywiii, kama mkinichagua nakwenda kuwatibia bure katika zahanati zote hospitali kubwa.”

Rais Samia Suluhu Hassana anaetetea kiti chake kupitia chama cha CCM aliahidi kujenga vituo zaidi vya afya.

“Tutaendelea kwa kasi ile ile katika huduma za afya, tutajenga vituo vya afya zaidi tutajenga zahanati zaidi na tunakwenda kuboresha hospitali yetu ya wilaya.”

Afya ni sekta mtambuka ikimgusa kila mwananchi, swali ambao wengi wanajiuliza Je ni kwa kiasi gani ahadi hizo zinawagusa wananchi lakini pia zinatekelezeka? Doreen Mlay na Mzamiru Nassoro ni wakazi wa Dar es Salaam.

Ni kwa kiwango gani ahadi hizo zinaweza kutekelezeka

“Tuseme kwamba sera hizi za afya katika majukwaa ya kisiasa katika mwaka huu wa uchaguzi wa 2025 zinakwenda kuleta mwanga mpya au mwanzo mpya katika huduma za afya iwe ni kwa watoa huduma iwe katika upatikanaji wa vifaa tiba iwe katika kuchangia gharama kati ya mgonjwa na serikali hiyo itaenda kuleta afya,” alisema Doreen.

“Amelenga maeneo mengine tofauti tofauti ikiwemo upatikanaji na usambazaji wa dawa na vifaa vya matibabu, kuna baadhi ya hospitali unaenda unakuta madaktari wapo, manesi wapo lakini sasa matibabu hayapatikaniki, yaani hakuna vifaa wala dawa kwahyo mgonjwa unapimwa unaambiwa ukachukue dawa dukani unaishia kwenda unapokujua wewe,” aliongeza kusema Mlay.

Dr Elisha Osati ni mtaalamu wa afya ya binadamu aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Madaktari nchini,anaziangalia ahadi hizo kwa upande wa kitaalamu.

Mitandao inaweza kushawishi kura yako?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

“Suala la bima ya afya kwa wote ni kwamba sheria yake imepita na kiukweli tunatamani utekelezaji uweze kutokea jinsi wanavyozungumza kwasababu gharama za matibabu zipo juu na watu wengi wetu hawawezi kulipa gharama za matibabu kwahyo ikiwepo bima ya afya kwa wote itatusaidia kutoa huduma bora kwa wananchi kwa gharama nafuu.”

Dokta Osati anayagusia mambo muhimu ambayo wananchi wanataka kuona katika sekta ya afya yanaboreshwa na serikali inayokuja.

“Wananchi wao wakija hospitali wanataka kuona wanapata huduma bora ambayo itatolewa kwa wakati kwa gharama nafuu ambayo inawapa nafasi ya kuweza kujieleza vizuri hatimaye kutibiwa kwa urahisi zaidi na kuweza kuondoka kwa haraka, hayo ndio matarajio ya wananchi, viongozi wetu ambao wanazungumza inamaana kwamba hilo ndio jambo kwanza wanalopaswa kuliweka katika vichwa vyao.”

Sekta ya afya imekuwa ajenda muhimu katika majukwaa ya kisiasa hususan katika kampeni za wagombea Urais kutokana na sekta hiyo kumgusa kila Mtanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *