#StarMgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga kwa kiwango…#StarMgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga kwa kiwango…

#StarMgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga kwa kiwango cha lami, Barabara ya Namanyere-Kizwite-Chelanganya katika Mji wa Namanyere mkoani Rukwa.

Sambamba na mradi huo, ameahidi kujenga soko la kisasa na stendi ya mabasi zinazoendana na hadhi ya Mji wa Namanyere mkoani humo.

Dkt Samia ametoa ahadi hizo leo, Jumamosi Oktoba 18, 2025 katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliofanyika Namanyere mkoani Rukwa.

Amesema Serikali yake itajenga Namanyere-Kizwite-Chelanganya na kuweka taa 270 za barabarani ili kuwawezesha wafanyabiashara wa eneo hilo, kufanya shughuli zao kwa saa 24.

Sambamba na barabara hiyo, amesema pia atajenga Barabara ya Mjimwema-Itekesya, kwa kiwango cha changarawe, huku akiwahakikishia wananchi wanaodai fidia zitalipwa baada ya uhakiki.

Kuhusu maji, amesema vyanzo vilivyopo wilayani Nkasi havikidhi mahitaji, hivyo wanakuja na mradi wa maji unaotoka Ziwa Tanganyika.

Pia, ameahidi kujenga stendi ya mabasi na soko la kisasa linaloendana na hadhi ya Mji wa Namanyere mkoani humo, ili kukuza fursa za biashara na uchumi kwa wananchi.
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *