Muasisi wa kampuni hiyo ni raia wa Afrika Kusini Thandoh Gumede, mwenye umri wa miaka 31, na mwalimu wa zamani katika eneo la vijijini la Hluhluwe mkoa wa KwaZulu Natal. Gumede anasema alianza kufanyia kazi mradi huo miaka minane iliyopita.

Mwalimu roboti anajibu anaposikia sauti, na kufanya mazingira ya masomo kuwa ya kuwasiliana na kuhamasisha wanafunzi, hasa katika maeneo ya vijijini.

Gumede ameweka lengo la kumfikisha roboti katika kila darasa Afrika Kusini, lakini amesisitiza kuwa itabidi washirikiane na wadau wengine katika maendeleo ili hilo litimie.

Wakati wa uzinduzi mjini Durban mwezi Agosti, Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Nomalungelo Gina, ameutaja ubunifu huo kama hatua muhimu ambayo “itawawezesha wanafunzi kutimiza malengo ya kupata mafunzo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *