Kovac aliyasema haya licha ya Bayern kutoshindwa katika mechi 10 katika mashindano yote msimu huu.
Kovac ambaye alichukua mikoba hapo signal iduna Park katikati ya msimu uliopita, ameipelekea Dortmund kutoshindwa katika mechi zake kwenye Bundesliga na Ulaya msimu huu.
Kwa sasa wanaishikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ujerumani,bundesliga, pointi nne nyuma ya mabingwa Bayern munich.
“Kwa sasa tuko imara na huo ndio msingi iwapo unataka kuwa na mafanikio yoyote yale. Bila shaka tunafahamu kwamba Bayern wako vizuri kwa sasa wamecheza mechi 10 na hawajashindwa katika mechi zote hizo,” alisema Kovac. “Wanachokifanya Bayern ni kzuri ila sisi nasi tuko katika mkondo mzuri na tuko tayari kabisa kuikabili hii changamoto.”
Mechi ya Jumamosi ni ya kwanza kati ya mechi sita za ugenini za Dortmund katika mechi zao saba zijazo kwenye mashindano yote zikiwemo mechi za Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya dhidi ya Copenhgane wiki ijayo na Manchester City mnamo Novemba 5.
Ila Kovac anasema hakuna haja ya kucheza kwa tahadhari huko Munich kwani wapinzani wao bayern, hutawala mechi kuanzia mwanzo hadi mwisho.
“Unapokuwa na hofu kidogo huko Munich, utapata wakati mgumu. Timu haziwezi kwenda kule na kujilinda tu, kwasababu wanafunga wastani wa mabao 4 kwa kila mechi. Lakini sisi nasi tuna wachezaji wazuri katika safu ya ushambuliaji na lazima tuwawekee shinikizo.”