Kikosi cha Wanaanga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimezindua makombora yaliyoboreshwa ya Emad na Ghadr katika miji ya makombora ya chini ya ardhi.

Makombora yaliyoboreshwa ya Emad na Ghadr ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la SEPAH yamezinduliwa wakati wa kipindi cha televisheni cha Jumamosi, kikionyesha miji ya makombora ya chini ya ardhi.

Kombora la balestiki la Ghadr linatumia vifaa vya kielektroniki vya kujibu mapigo kwa kasi. Kombora la Emad pia limeboreshwa na limeongezewa kasi na nguvu.

Kombora la masafa marefu la Emad, ambalo ni toleo lililoboreshwa la Ghadr, lina mfumo wenye usahihi ulioimarishwa wa kulenga shabaha.

Kwa mujibu wa maafisa wa jeshi la Iran, Emad lina uwezo wa kuongozwa kwa mbali hadi kufikia kenye shabaha, na hivyo kulifanya kuwa kombora la kwanza la Iran linaloongozwa kwa usahihi wa hali ya juu.

Kombora la Ghadr, ni kombora la hatua mbili, likiwa na hatua ya kwanza inayoendeshwa na mafuta ya kioevu na hatua ya pili inayoendeshwa na mafuta mango. Kuna aina tatu za kombora la Ghadr:  Ghadr-S lenye masafa ya kilomita 1,350, Ghadr-H lenye kilomita 1,650, na Ghadr-F lenye kilomita 1,950.

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran aliashiria uwezo wa kustaajabisha wa vijana wa Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, vijana wa taifa hili ndio ambao wanatengeneza makombora na nishati ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutegemea uwezo wa ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *