
Chanzo cha picha, Goal.com
Meneja wa Celtic, Brendan Rodgers anatarajiwa kuzungumza na Nottingham Forest wakati timu hiyo ikimuondoa maneja wao Ange Postecoglou. (Football Insider)
Chelsea wanaonekana kuwa mstari wa mbele kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 23 kutoka kwa wapinzani wao wa ligi kuu England Aston Villa. (Caught Offside)
Real Madrid wamewataja mabeki watatu ambao watatarajia kuwasajili mwaka ujao, ambao ni mchezaji wa kimataifa wa Uingereza wa Crystal Palace, Marc Guehi, 25, beki wa kati wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano, 26, na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na Liverpool Ibrahima Konate, 26. (Talksport)
Manchester City, Chelsea, Liverpool na Arsenal wote wanavutiwa na winga wa River Plate, Muargentina, Ian Subiabre, 18, ambaye anatarajiwa kuhamia Ligi Kuu ya England mwaka ujao. (TBR Football)
Nottingham Forest bado wanamfikiria meneja wa Fulham, Marco Silva – pamoja na Sean Dyche na Roberto Mancini – kama chaguo kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou aliyetimuliwa. (Guardian)

Chanzo cha picha, Goal.com
Mshambulizi wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 19, Endrick ana nia ya kuhamia Marseille kutokana na kukosa muda wa kucheza katika klabu hiyo ya La Liga. (L’Equipe)
Tottenham, Chelsea na Manchester United wako katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 25 kutoka Juventus. (Football Insider)
Chelsea huenda ikataka kumnunua tena kiungo wa kati wa Ubelgiji, Diego Moreira, 21, kutoka klabu ya Strasbourg. (TBR Football)
Real Madrid wanafuatilia maendeleo ya kiungo wa kati wa Mexico, Gilberto Mora, 17, anayechezea klabu ya Mexico ya Tijuana. (AS)