
Mamlaka ya ulinzi wa raia ya Ukraine imeripoti kuharibiwa kwa majengo kadhaa mjini Shakhtarske katika mkoa wa Dnipropetrovsk, umbali wa kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu wa eneo hilo, Dnipro.
Watu 10 wajeruhiwa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine
Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, gavana wa mkoa huo Vladyslav Hayvanenko amesema kuwa watu 10 walijeruhiwa.
Mjini Moscow, wizara ya ulinzi ya Urusi imeripoti kudungua droni 45 za Ukraine nyingi zikinaswa katika maeneo ya Samara na Saratov kando ya Mto Volga. Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya uharibifu ama majeruhi.