
Wakati wa maandamano mjini Rome, makumi ya wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara walielezea kile walichopitia Libya, na kimya cha dakika moja kikadumishwa kwa heshima ya wale waliokufa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania.
Mamia ya watu walihudhuria hafla hiyo, akiwemo mwanaharakati Sarita Fratini.
Fratini amekuwa akisaidia wahamiaji kuishtaki Italia baada ya kukamatwa katika bahari ya Mediterania na Libya na kurudishwa katika vituo vya kizuizini katika eneo hilo.
Wanaharakati wa haki na wafungwa wa zamani wameshutumu vituo kama hivyo kwa unyanyasaji, mateso na uhalifu mwingine.
Katika miezi ya hivi karibuni, mashirika yasiyo ya kiserikali yameripoti kuongezeka kwa matukio ya walinzi wa pwani wa Libya kushambulia kwa risasi boti zilizokuwa zimebeba wahamiaji katika bahari ya Mediterania.