
Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe kilitangaza Jumamosi kwamba kitaanza hatua za kuongeza muda wa uongozi wa Rais Emmerson Mnangagwa kwa miaka miwili, hatua ambayo inaweza kumuweka madarakani hadi mwaka 2030.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zimbabwe, Mnangagwa anatarajiwa kuondoka madarakani mwaka 2028 baada ya kumaliza vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja. Mabadiliko yoyote ya kuongeza muda yatahitaji marekebisho ya vifungu vya ukomo wa muda wa uongozi.
Azimio hilo, lililopitishwa katika mkutano wa kila mwaka wa chama hicho uliofanyika katika mji wa Mutare, mashariki mwa nchi, linaelekeza serikali “kuanzisha marekebisho ya kisheria yanayohitajika” kutekeleza mpango huo, alisema Waziri wa Sheria Ziyambi Ziyambi, ambaye pia ni katibu wa masuala ya kisheria wa ZANU-PF.
Mamia ya wajumbe walishangilia wakati azimio hilo lilipopitishwa.