Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya ziwa Ezekiel Wenje amewaomba Watanzania kumpigia kura Mgombea Urais kupitia Chama Cha M…Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya ziwa Ezekiel Wenje amewaomba Watanzania kumpigia kura Mgombea Urais kupitia Chama Cha M…

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya ziwa Ezekiel Wenje amewaomba Watanzania kumpigia kura Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi Mkuu wa Octoba 29 mwaka huu.

Wenje ametoa ujumbe huo October 18/2025 alipokuwa kwenye kampeni za Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Mpanda Mkoani Katavi ambapo amesema Kwa takwinu za miradi iliyotekelezwa ndani ya miaka minne inaomesha dhamira ya kweli ya CCM ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Wenje ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Nyamagana amesema Dkt Samia Suluhu Hassan alipoingia Madarakani amefanya kazi kubwa ya kufanya Maridhiano na vyama na upinzani na marekebusho ya sheria yakafanyika lakini vyama vya upinzani Bado vinabeza juhudi hiyo.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *