#HABAI: Benki ya CRDB imeingia Ubia wa kimkakati wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 300 na Taasisi tatu za Kimataifa, ili kukuza ujasiriamali, kuimarisha biashara na kuboresha makazi katika mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Mikataba hiyo imesainiwa kwenye Jukwaa la Wabia na Wawekezaji lililofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Jijini Washington nchini Marekani.

Mikataba hiyo kati ya Benki ya CRDB na FinDev Canada, DEG (KfW Group) ya Ujerumani na Shelter Afrique Development Bank, imesainiwa katika Jukwaa la Wabia na Wawekezaji lililoandaliwa na Benki ya CRDB, kujadili fursa za uwekezaji nchini Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kueleza namna Benki ya CRDB imejipanga kuwawezesha wawekezaji kuzitumia fursa zilizopo katika mataifa hayo.

Katika makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki yetu ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema FinDev Canada imewekeza Dola za Marekani Milioni 60 (Shilingi Bilioni 150) kusaidia miradi ya wajasiriamali hususani wanawake na vijana, na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wakati DEG (KfW Group), ikiwekeza Dola Milioni 50 (Shilingi Bilioni 125) kuimarisha Biashara ndogo na za kati pamoja na kuchochea ajira kwa vijana.

Kwa upande wa Shelter Afrique Development Bank, imewekeza Dola Milioni 10 (Shilingi Bilioni 25) ili kuendeleza makazi bora na nafuu nchini DRC.

Katika hafla hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Tanzania, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, walihudhuria viongozi wa serikali kutoka mataifa ambako Benki ya CRDB inatoa huduma zake, akiwamo Waziri wa Fedha wa Burundi, Waziri wa Habari wa DRC, Magavana wa Benki Kuu za Tanzania na Burundi, na Mabalozi wa Tanzania na Burundi nchini Marekani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *