#HABARI: Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imepokea karatasi za kupigia kura 717,557 kutoka kwa wakala wa uchapaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa ajili ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika terehe 28 na 29 ya mwezi huu wa Oktoba Kisiwani humo.
Karatasi hizo zimepelekwa katika Ofisi za Tume hiyo chini ya Ulinzi mkali wa Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliokuwepo katika magari makubwa ya Jeshi hilo.
Mara baada ya Karatasi hizo kukabidhiwa, Mkurugenzi wa ZEC Bw.Thabit Faina Idarous na Mwakilishi wa Wakala wa uchapaji walitia saini hati ya makabidhiano.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walioshuhudia tukio hilo wamesema huo ni muendelezo mzuri wa kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Karatasi hizo zimegharimu shilingi Milioni 908, 327,300 chini ya Bajeti iliyopangwa ya Shilingi 1,245,592,000.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.