Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bethsaida wameomba msaada wa kuunganishiwa maji safi, kupata chakula cha kutosha na vifaa vya kufundishia masomo ya sayansi, kutokana na uhaba mkubwa unaowakwamisha kujifunza vizuri.

Wanafunzi hao, ambao wamemaliza kidato cha nne, wanasema kuwa kwa sasa ni changamoto kupata maji safi ya kunywa, na kuwa vifaa vya sayansi ni vichache, jambo linalowalazimu kutumia muda mfupi sana kujifunza kwa ufanisi.

Shule hiyo awali ilikuwa ni kituo cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza kabla ya kubadilishwa na kuwa kuwa shule ya sekondari, na kwa mujibu wa mkuu wa shule, wengi wa walimu waliopo wanasimamia masomo kwa kujitolea.

✍ Esterbella Malisa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *