
Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumapili jioni, Oktoba 19, kwamba litasitisha mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa usitishaji mapigano, baada ya kutekeleza makumi ya mashambulizi mabaya, yanayodaiwa kulenga maeneo ya Hamas, ambayo inayoshutumiwa kwa mashambulizi dhidi ya wanajeshi wake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kwa mujibu wa maagizo kutoka kwa safu ya kisiasa, na baada ya mfululizo wa mashambulizi muhimu katika kukabiliana na ukiukaji wa Hamas,” jeshi “limeanza tena utekelezaji wa usitishaji vita,” limesema katika taarifa yake.
Jeshi la Israel “litaendelea kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na litajibu kwa uthabiti ukiukaji wowote,” imeongza taarifa hiyo.
Wakati huo huo Shirika la Ulinzi la Raia la Gaza limetangaza kwamba mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya takriban watu 33. Ripoti ya awali ilisema idadi ya waliouawa ni takriban 11. Miongoni mwa wahasiriwa ni watu sita waliouawa katika shambulio la Israel huko Al-Zawaida, katikati mwa eneo hilo, kwenye “kundi la raia,” wote waliohamishwa kutoka maeneo ya kaskazini, amesema Mahmoud Bassal, msemaji wa Shirika la Ulinzi wa Raia.
Hamas, kwa upande wake, imehakikisha kwamba haifahamu mapigano yoyote katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza na kusisitiza kwamba maeneo hayo yamesalia “chini ya udhibiti” wa Israel. Hamas ambayo kimethibitisha tena wakati huo huo “dhamira yake kamili ya kutekeleza kila kitu ambacho kimekubaliwa,” imeshutumu Israel kwa “kubuni visingizio” vya kuanzisha tena mashambulizi yake huko Gaza.
Kuibuka tena kwa ghasia hizo kunafuatia matamshi ya Benjamin Netanyahu siku ya Jumamosi, ambaye alibainisa juu ya kupokonywa silaha kwa Hamas kama sharti la kumaliza vita, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kuhusu suala la kubadilishana miili kati ya Israel na Hamas.