Kijana Issa Mfaume (31), ambaye kwa muda mrefu amekuwa kitandani kutokana na changamoto za kiafya baada ya kuangukiwa na gogo akiwa kwenye shughuli za kuchana mbao mwaka 2014, ameonesha mfano wa kuigwa kwa kutumia ujuzi wake wa kurekebisha simu na vifaa vyake kama chanzo pekee cha matumaini na kipato.

Ajali hiyo iliyomsababishia majeraha makubwa katika eneo la kiuno imemfanya Issa kushindwa kutembea, lakini haikumkatisha tamaa ya kuendelea kujitafutia riziki kwa njia halali.

Akiwa katika mazingira magumu, Issa ameendelea kutumia kipaji chake katika urekebishaji wa vifaa vya kielektroniki, hatua inayomsaidia kujitegemea na kuhamasisha vijana wengine kutokata tamaa licha ya changamoto za maisha.

✍ Omary Mikoma
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *