Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetoa wito kwa walimu kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, sambamba na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia.

Rais wa CWT, Dkt. Selemani Ikomba, amesema walimu wana nafasi ya kipekee katika jamii kama walezi na viongozi wa fikra, hivyo ni wajibu wao kutumia nafasi hiyo kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura kama njia halali ya kuchagua viongozi wanaowataka.

✍ George Mbara
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *