
Rais wa Marekani, Donald Trump amemshutumu Rais wa Colombia Gustavo Petro kwa kuhusika katika kuongezeka biashara ya dawa za kulevya, na kutishia kuingilia moja kwa moja Marekani nchini Colombia.
Trump amemtuhumu mwenzake wa Colombia, Gustavo Petro, kuwa “anahimiza uzalishaji mkubwa wa dawa za kulevya” nchini humo, akimtaja kama “mtawala haramu wa biashara ya dawa za kulevya.”
Donald Trump amedai kuwa Rais Gustavo Petro hafanyi jitihada za kusitisha biashara haramu ya dawa za kulevya. Trump ametishia kwamba Marekani itaingilia moja kwa moja nchini Colombia tena kwa njia isiyokuwa nzuri.
Kwa upande wake Rais wa Colombia, Gustavio Petro amedokeza kuwa Trump anapotoshwa na chama na washauri wake na kuongeza kuwa, “Yeye ndiye adui mkubwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini humo katika karne ya 21.
Gustavio Petro amesema “Trump ni mkorofi na hajui lolote kuhusu Colombia.”
“Ninapendekeza kwamba Trump asome kuhusu Colombia na kuamua ni wapi wanasimama walanguzi wa dawa za kulevya na wapi wanasimama wanademokrasia,” Petro ameongeza.
Waziri wa Ulinzi wa Colombia, Pedro Sanchez pia amejibu matamshi ya Trump akisema, “Hii ni dharau kwa Colombia.”