
Hii ni baada ya kusitisha shughuli hiyo kufuatia kile ilichokitaja kuwa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya vikosi vyake. Mashambulizi hayo yaliua watu wawili. Vyanzo vya usalama vimesema hayo siku ya Jumatatu.
Kulingana na afisa wa usalama wa Israel, uongozi wa kisiasa umeamuru misaada ya kibinadamu iruhusiwe kuendelea kuingia Gaza kupitia kivuko cha Kerem Shalom na vivuko vingine kulingana na mkataba kati yao na wanamgambo wa Hamas.
Mnamo Jumapili, vyanzo vya usalama vilisema upelekaji misaada Gaza ulisimamishwa kwa sababu Hamas walikiuka kwa makusudi makubaliano ya usitishaji vita
Kulingana na jeshi la Israel, wanajeshi wake walioko kusini mwa Ukanda wa Gaza walishambuliwa na wawili waliuawa.
Israel ilijibu kwa kufanya mashambulizi makubwa zaidi ya angani tangu mkataba wa usitishaji vita uliposainiwa Oktoba 10.
Vyanzo vinaeleza kuwa watu 44 waliuawa kwenye shambulizi hilo la Israel.