
Rais wa Urusi, Vladmir Putin na mwenzake wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, hivi leo walikuwa wageni waheshima katika sherehe za gwaride kubwa la kijeshi lililoandaliwa na Uchina kwenye mji wa Beijing, ikiwa ni kumbukizi ya miaka 80 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa za kimataifa, China kuwaalika Putin na Kim kunatuma ujumbe kwa Marekani na washirika Wake kuwa, kuna muungano mwingine wa nchi nyingine zenye nguvu ya nyuklia zinazoweza kuja pamoja na kukubaliana.
Katika hotuba yake kwa maelfu ya raia na wanajeshi walioshiriki sherehe za hivi leo, rais Xi Jinping amesema ‘China haizuiliki’ na kwamba nchi yake itakuwa mstari wa mbele kutafuta amani ya dunia kupitia diplomasia na kwamba haitatishwa na taifa jingine, akitaka mataifa kuungana.
Katika hatua nyingine, rais wa Marekani, Donald Trump, amewatuhumu viongozi wa Uchina, Korea kaskazini na Urusi kushirikiana kupanga njama dhidi ya taifa lake, akituma salamu kwa rais Putin na Kim Jong Um.
Mamilioni ya raia wa China waliuawa wakati wa vita ya China na Japan katika miaka ya 1930 na 40, vita ambayo ilikuja kuwa sehemu ya mzozo mkubwa wa kimataifa kufuatia shambulio la Tokyo kwenye Bandari ya Pearl mwaka 1941.