#HABARI: Mgombea ubunge Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anjellah Kairuki ameendelea na kampeni zake katika Kata ya Msigani na kubainisha vipaumbele vyake kumi ikiwemo kusimamia suala la urasimishaji ardhi na kushughulikia migogoro ya ardhi endapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Ameyasema hayo wakati mkutano wa kampeni uliofanyika Msigani, Ubungo jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa atasimamia ujenzi wa vituo vya polisi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao, pamoja na kuanzisha vituo vya afya vitakavyoboreshwa ili kuhudumia wakazi kwa ukaribu sambamba na ujenzi wa masoko ya uhakika, hususan kwa wafanyabiashara wadogo.

Aidha, Kairuki ameendelea kutaja vipaumbele vingine ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara kuu na za ndani ili kuongeza mtandao wa usafirishaji, pamoja na ujenzi wa madaraja na vivuko kwa maeneo yanayohitaji huduma hizo na kuwataka wananchi wa Kibamba kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kupiga kura na kumchagua ili aweze kutekeleza ahadi hizo kwa manufaa ya maendeleo ya jimbo na Taifa kwa ujumla.

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *