Wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tingatinga, wilayani Longido, mkoani Arusha, wameeleza kupata matumaini mapya kuhusu elimu ya amali baada ya wanafunzi wa shule hiyo kubuni njia ya kutengeneza virutubisho vya maziwa ya ng’ombe.

Wazazi wamesema ubunifu huo unaweza kuwa msaada mkubwa kwa ndama wanaopoteza mama zao kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ukame na magonjwa ya mifugo.

Shule ya Tingatinga, ambayo ipo katika jamii za kifugaji, imekuwa mfano wa utekelezaji wa elimu ya amali kupitia somo la kilimo na ufugaji. Kupitia mfumo huo, wanafunzi wamefanikiwa kuunda “Artificial Colostrum”, virutubisho vinavyofanana na vile vinavyopatikana kwenye maziwa ya mama wa ndama, wakitumia mbinu za kisayansi na ubunifu wa vitendo.

✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *