Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa Rais, atahakikisha anasimamisha huduma za mikopo umiza maarufu kama “Kausha damu” ambapo atahakikisha serikali yake inawekeza mawazo ya biashara katika sekta zinazotambulika na serikali kama vile Benki, ili kuwaondolea wananchi adha ya kuporwa vitu bila ya kufuata taratibu.
✍Alpha Jenipher
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates