
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali matamshi ya hivi karibuni ya Rais Donald wa Marekani kuhusu Iran na eneo la Asia ya Magharibi na na kusema, Trump alisafiri hadi Palestina iliyokaliwa kwa mabavu na kutoa maneno matupu yenye kejeli ili kuwatia moyo Wazayuni waliokata tamaa.
Akizungumza leo asubuhi katika hadhara ya mamia ya vijana wa Iran waliopata medali katika mashindano ya michezo na ya kielimu ya kimataifa, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliwapongeza vijana hao na kuwataja kama nembo ya nguvu ya kitaifa na ushahidi wa uwezo wa vijana wa Kiirani katika kuinua jina la Iran kileleni ulimwenguni.
Kiongozi Muadhamu amesema: “Rais wa Marekani alijaribu kuonyesha uongo na tabia za kipuuzi ili kuwapa Wazayuni matumaini, lakini kama ana uwezo, basi aende akawatulize mamilioni ya raia wa Marekani wanaoandamana dhidi yake katika majimbo yote ya nchi hiyo.”
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, Iran ilitoa mshituko mkubwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 12, ambapo makombora yaliyotengenezwa na vijana wa Kiirani yalipenya ndani kabisa ya maeneo nyeti ya adui na kuyafanya kuwa majivu.
“Makombora haya hayakunuliwa wala kukodishwa — ni matunda ya juhudi na akili ya vijana wa Kiirani,” alisema. “Wakati kijana wa Kiirani anapoingia uwanjani kwa bidii na elimu, anaweza kufanya mambo makubwa kama haya.”
Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa vikosi vya ulinzi vya Iran vina uwezo kamili wa kutumia tena silaha hizo wakati wowote inapohitajika.
Kadhalika Ayatuullah Khamenei amesema, “Katika vita vya Gaza, Marekani ndiyo mshirika mkuu wa jinai za utawala wa Kizayuni, kama alivyokiri mwenyewe kwamba ‘tulikuuwa tukifanya kazi pamoja na Israel katika vita vyaGaza.’ Silaha na mabomu yaliyomiminwa juu ya watu wasio na hatia yalitoka Marekani.”
Akimjibu bwabwaja za Trump aliyedai kuwa anapambana na ugaidi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: “Zaidi ya watoto na wachanga elfu ishirini wameuawa Gaza — je, hao ni magaidi? Magaidi wa kweli ni Marekani, ambao waliunda kundi la Daesh (ISIS) na kulitumia kuleta machafuko katika eneo hili.”
Ayatollah Khamenei alisema kuwa vifo vya watu takribani 70,000 Gaza na mauaji ya zaidi ya Wairani 1,000 katika vita vya siku 12 ni ushahidi wa asili na dhjati ya kigaidi ya Marekani na Israel. “