Mkutano huo haukuripotiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari duniani lakini idara ya usalama ya Urusi, FSB, ililifuatilia kwa umakini sana azimio hilo la Bunge la Baraza la Ulaya (PACE). Kwa Kremlin, wapinzani wa Putin waliokimbilia uhamishoni ni kama wamepotea tu lakini kiuhalisia bado hawajasahaulika.

Bila kusubiri jukwaa hilo la Usalama litaje majina ya washirika wa Urusi, tayari Idara ya Idara ya usalama ya urusi, FSB imeitumia nafasi hiyo  kuwa ni sababu muhimu ya kuanzisha uchunguzi mpya wa makosa ya jinai kwa wapinzani 23 walioko nje ya nchi, ambao wanatuhumiwa kwa kuanzisha kundi la kigaidi na kupanga njama za kuiangusha serikali ya Moscow.

Tajiri wa zamani wa mafuta huko Urusi, Mikhail Khodorkovsky alitajwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililopo uhamishoni amesema yeye angependa kuwa sehemu ya wajumbe wa baraza hilo la mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Putin na wakosoaji wake walio uhamishoni.

Khodorkovsky, kwa sasa anaishi uhamishoni jijini London, Uingereza mwanzoni mwa miaka ya 2000 alifungwa jela kwa miaka 10 kwa mashtaka ya ulaghai na hukumu yake hiyo ilikosolewa vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliyodai kuwa ilitokana na msukumo wa kisiasa.

Dmitri Peskov msemaji wa Kremlin
Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov Picha: Sefa Karacan/dpa/TASS/picture alliance

Urusi yasema kuna maadui wanaofanya harakati za kutaka kuiangusha serikali

Wakati huo huo wapinzani wa Putin waliopo uhamishoni pamoja na kukubaliana na maazimio ya Baraza la bunge la Ulaya juu ya kuundwa kwa jukwaa la mazungumzo bado hawajawa na uhakika wa moja kwa moja wa usalama wao, huku Putin mwenyewe akionekana kuwatilia shaka na hata kuanzisha uchunguzi dhidi ya wanaotuhumiwa kufanya njama za kuiangusha serikali yake.

Alipoulizwa na shirika la habari la Reuters ikiwa Urusi ilikuwa na wasiwasi na ushiriki wa Khodorkovsky na wengine katika jukwaa hilo,msemaji wa ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov alijibu kuwa ndani na nje ya Urusi kumekuwa na maadui wanaofanya harakati za kutaka kuiangusha serikali na kutishia kuchukua hatua zinazofaa kwa yeyote atakaebainika kuwa na mpango ovu dhidi ya serikali ya Moscow.

Tangu kuanguka kwa muungano wa nchi za kisoviet, wakosoaji wengi wa serikali ya Urusi walijikuta katika wakati mgumu na wengi walilazimika kukimbilia uhamishoni na muda wote idara ya usalama ya Urusi imekuwa ikiwatazama kama watu ama kundi lenye nia ovu na serikali ya Moscow.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *