
Yanga imewatoa wito kwa mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi, Oktoba 25, 2025 ili kuipa hamasa timu hiyo iweze kuibuka na ushindi dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.
Katika mchezo huo, Yanga inahitaji ushindi wa tofauti ya mabao mawili au zaidi ili iweze kusonga mbele baada ya kupoteza mechi ya kwanza kwa bao 1-0.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa uwepo wa idadi kubwa ya mashabiki Jumamosi, utasaidia kuongeza morali kwa wachezaji na hivyo kuiweka katika mazingira mazuri ya kupata ushindi mnono.
“Ndugu zangu Wanayanga wenzangu, hii kwetu ni zaidi ya dakika 90. Hii kwetu ni zaidi ya mechi ya kawaida. Hii ni mechi ambayo inabidi tuichukue timu yetu, tukaipambanie tuipeleke katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
“Inawezekana kabisa kwa umoja wetu, kwa dua zetu, kwa sala zetu, kwa nguvu zetu na sauti zetu ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, Young Africans tunao uwezo wa kupindua matokeo. Lakini huu uwezo, unaanza na wewe mwanachama mwenzangu, mshabiki mwenzangu wa Young Africans.
Tukiweka jitihada, tukienda kupambana kwa pamoja, tutakwenda kufurahi kwenye ardhi yetu ya nyumbani, Dar es Salaam Tanzania. Mjulishe na mwananchi mwenzako. Mjulishe na rafiki yako, mwambie mechi ya kufuzu imefika, mimi na wewe tunahitajika Benjamin Mkapa kuipeleka Yanga yetu hatua ya makundi,” amesema Kamwe.
Kauli ya Kamwe imeunga mkono na nyota wa Yanga ambao wamewaomba mashabiki wa Yanga kwenda kuwasapoti na watahakikish hawawaangshi.
“Tumeumizwa lakini tumejifunza na hata tulipokutana, tumekubaliana tunarudi nyumbani kubadilisha. Hii ni timu ambayo tumewahi kushinda pale ambapo ilionekana hatutaweza kushinda. Tulifanya ugenini na hata nyumbani tunakwenda kufanya kweli. Tunawaomba mashabiki wasikate