#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na askari wa Wanyamapori limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne waliokuwa wakijihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali, ambapo walikutwa na meno 23 ya tembo pamoja na kichwa cha mnyama aina ya swala.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 19, 2025 akiwa Wilaya ya Kilombero, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro alisema kuwa, operesheni hiyo ni sehemu ya jitihada za kudhibiti uhalifu wa wanyamapori na kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa.
Aidha, Kamanda alisema watuhumiwa wengine wawili wa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, waliotekeleza tukio la wizi wa pikipiki, nao wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na Polisi.