Mgombea wa urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema anatambua changamoto ya msongamano wa magari katika barabara ya Kilwa, hususan kipande cha Kongowe hadi Mbagala Rangitatu, na ameahidi kuangalia uwezekano wa kupanua barabara hiyo ili kupunguza foleni kubwa ya magari.
Akizungumza leo, Jumatatu Oktoba 20, 2025, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mkuranga, mkoani Pwani, Dkt. Samia amesema kuwa msongamano huo umekuwa ukilemaza shughuli za usafiri, usafirishaji, biashara na maendeleo ya kijamii katika Mkoa wa Pwani na mikoa jirani, hivyo serikali ijayo italipa kipaumbele suala hilo.
Aidha, Dkt. Samia alizungumzia mpango wa ujenzi wa barabara ya Mkuranga Mjini hadi Kisiju yenye urefu wa kilomita 40, akibainisha kuwa serikali itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutokana na umuhimu wake kiuchumi.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates