YANGA SC: “…tumeteleza, lakini bado hatujaanguka”
Yanga SC tayari wametua Dar es Salaam usiku huu wakitokea nchini Malawi kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers.
Kabla ya kuondoka nchini humo, kikosi hicho kilipiga tizi la kuweka sawa milii ya wachezaji kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumamosi hii….
Katikati ya tizi hilo, Meneja Habari na Mawasiliano, Ally Kamwe anatoa ujumbe kwa mashabiki wa timu hiyo akiwaeleza kwamba wachague moja; ama kukaa nyumbani timu iishie hatua za awali, au wajae dimbani timu ifuzu hatua ya makundi…
Kamwe anasema Jumamosi ni zaidi ya dakika 90 za kawaida “…Jumamosi ni mechi ya kufuzu”
#YangaSC #CAFCL #AllyKamwe