Mwezi Septemba, mahakama ya Ufaransa ilimkuta Sarkozy na hatia ya kula njama za uhalifu katika kesi inayohusiana na juhudi zake za kujipatia fedha kinyume cha sheria ili kufadhili kampeni yake ya uchaguzi wa mwaka 2007, fedha zilizotoka kwa mtawala wa Libya wakati huo Muammar Gaddafi.

Nicolas Sarkozy  ambaye atakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa na hata katika Umoja wa Ulaya kwenda jela, alipokelewa wiki iliyopita na rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysée, lakini mazungumzo yao hayakuwekwa wazi. Mawakili wa Sarkozy aliyeiongoza Ufaransa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, wametangaza kuwa watawasilisha mara moja ombi la kuachiliwa kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *