Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu ameonya kwamba Hamas “itatokomezwa” ikiwa itakiuka makubaliano ya Gaza na Israel, lakini akasema itapewa fursa ya kuheshimu makubaliano hayo. Makamu wa Rais J.D. Vance amesafiri hadi Israel muda mfupi baadaye, akijiunga na wajumbe wa Marekani, huku ghasia za mwishoni mwa wiki iliyopita zikitishia makubalino ya usitishaji mapigano.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tumefanya makubaliano na Hamas: Watatii makubaliano hayo, watakuwa na tabia nzuri, na watakuwa mwenendo mzuri,” Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House alipokuwa akimpokea Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese.

“Na ikiwa watakiuka makubaliano ya sitishaji vita, tutachukuwa hatua na kuwaangamiza, ikiwa ni lazima. Watatokomezwa, na wanajua.”

Trump alichangia mazungumzo ya makubaliano ya Gaza karibu wiki mbili zilizopita, lakini makubaliano hayo yamekuwa katika tishio la mara kwa mara, huku Israel ikiishutumu Hamas kwa kuchelewesha kuwakabidhi mateka waliouawa na kuanzisha mashambulizi.

Kiongozi mkuu wa ujumbe wa Hamas katika mazungumzo, Khalil al-Hayya, ameliiambia Gazeti la Al-Qahera News la Misri kwamba kundi hilo limesalia kujitolea kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

“Tunaona ni vigumu sana kutoa miili, lakini tuko makini na tunafanya bidii kuitoa,” amesema katika hotuba yake iliyorushwa leo Jumanne asubuhi.

“Mkataba wa Gaza utatekelezwa, kwa sababu tunataka ufanyike, na tuko tayari kuuheshimu.”

Trump pia ameonya kundi hilo la wanamgambo kuacha kuwanyonga hadharani wanaoshukiwa kuwa wapinzani na washirika wake huku likijaribu kurejesha udhibiti wa eneo hilo lililoharibiwa.

Trump amesisitiza, hata hivyo, kwamba vikosi vya Marekani havitashiriki katika makabiliano na Hamas, akisema kuwa makumi ya nchi ambazo zimekubali kujiunga na kikosi cha kimataifa cha kuleta utulivu huko Gaza “zingefurahi kuingilia kati.”

“Zaidi ya hayo, Israeli itaingilia kati kwa dakika mbili ikiwa nitaiomba,” Trump amesema.

“Lakini hivi sasa, hatujasema hivyo. Tutatoa nafasi kidogo, tunatumai kutakuwa na vurugu kidogo. Lakini sasa hivi, unajua, hawa ni watu wenye jeuri,” ameongeza.

“Wamekuwa wakaidi sana na wamefanya mambo ambayo hawakupaswa kufanya. Ikiwa wataendelea, tutaingilia kati na kutatua hali hiyo, na itafanyika kwa haraka sana na kwa vurugu.”

Trump amesema Hamas sasa ni dhaifu zaidi, haswa kwa vile Iran, mtetezi wa kikanda, haiwezekani kuingilia kati kwa niaba yake baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli mwaka huu.

“Hawana uungwaji mkono wa mtu yeyote tena. Lazima wakubaliane na hali, na wasipofanya hivyo, watatokomezwa,” Trump amesisitiza.

Mjumbe maalum wa Trump, Steve Witkoff, na mkwe wake, mshauri Jared Kushner, walikutana na Netanyahu siku ya Jumatatu kujadili “maendeleo na habari za hivi punde katika eneo hilo,” msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *