Mashirika ya ndege ya Qatar Airways na Kenya Airways yametangaza kuzindua mfumo wa ushirikiano utakawaofikisha wateja wao katika maeneo 19, huku maeneo mengine yakitarajiwa kuongezwa hivi karibuni.
Abiria wa Kenya Airways sasa wanaweza kuunganisha safari zao katika miji kumi kati ya Nairobi na Doha, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad.
Vilevile, wateja wa shirika la ndege la Qatar Airways wanaweza kufika katika maeneo nane kwa kutumia mtandao wa Kenya Airways, kutokana na safari tatu za ndege za kila siku kati ya Doha na Nairobi. Wateja wataweza kusafiri kwa kutumia mfumo huu kuanzia tarehe 26 Oktoba 2025.