Hii ni kufuatia jeshi kuchukua madaraka wiki iliyopita hatua iliyosababisha Rais Andriy Rajoelina kuikimbia nchi.

Kufuatia mashauriano na bunge, Randrianirina amemchagua Herintsalama Rajaonarivelo kama waziri mkuu mpya. Rajaonarivelo ni mtu mwenye ushawishi katika sekta binafsi nchini humo na mwenyekiti wa zamani wa benki ya Madagascar, Malagasy Bank BNI.

Rais Randrianirina ambaye aliapishwa Ijumaa, ameahidi kuunda serikali ya kiraia na ushirikiano na nguvu zote zinazoiendesha nchi hiyo baada ya jeshi kuchukua madaraka.

Amekanusha madai yaliyoibuka wiki iliyopita kwamba aliongoza mapinduzi. Maandamano ya mwezi uliopita ya kupinga hatua ya kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini humo, yaligeuka haraka na kuwa maandamano makubwa ya kuipinga serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *