Mwanasiasa mashuhuri, Sanae Takaichi (64) amechaguliwa kuwa waziri mkuu wa Japan; na hivyo kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu katika historia ya taifa hilo, linalotawaliwa kwa wingi na wanaume wenye umri mkubwa kuanzia ngazi za chini hadi serikalini.

Unaweza kuita ni kuvunja miiko au kuteketeza ukuta, ama kusema ni nyakati mpya kwenye historia ya taifa la Japan, ambapo waziri wa usalama na uchumi, mtangazaji wa televisheni na mpiga ngoma wa zamani, sasa anachukua jukumu kubwa la kuongoza nchi, inayopitia mipasuko ya kiuchumi na kisiasa.

Takaichi anaingia katika jukumu hilo, wakati ambao Japan inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi hususan mfumuko wa bei pamoja na changamoto za kisiasa, ikiwa ni siku chache kabla Rais wa Marekani Donald Trump hajazuru nchini humo.

Oktoba 04, 2025 Takaichi alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama tawala cha Liberal Democratic Party (LDP) , akichukua nafasi ya Shigeru Ishiba aliyejiuzulu nafasi hiyo sambamba na wadhifa mkubwa zaidi wa kitaifa nchini humo (waziri mkuu).

Chanzo | Reuters, BBC
📷 AFP
✍ @abuuyusuftz

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *