Hatua hii inatishia uchunguzi muhimu na juhudi za uwajibikaji. Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Huduma ya haki za kibinadamu, ISHR.

Shirika hilo linasema hatua ya Marekani kutolipa ada yake ya uanachama ya Umoja wa Mataifa pamoja na juhudi za China na Urusi kuondoa ufadhili wa mashirika ya kuetetea haki, ni mambo yanayoweza kuwa pigo kwa mapambano ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya ukiukaji wa haki.

Shirika hilo pia limesema kuwa tayari uchunguzi wa ngazi ya juu ulioamrishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kuhusiana na machafuko yanayoikumba Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, umeshindwa kufanyika kutokana na ukosefu wa fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *