Vyuo Vikuu saba vya juu nchini Marekani vimepinga mpango tata wa “kielimu” wa Ikulu ya White House, ambao unashutumiwa kuwa ni mkakati wa kisiasa unaolenga kuwanyamazisha wapinzani na kuwaadhibu wanaoiunga mkono Palestina katika Vyuo Vikuu.

Chuo Kikuu cha Arizona ni taasisi ya taaluma ya Marekani ambayo hivi karibuni imepinga matakwa ya sera mpya ya serikali yaTrump, na kukataa ufadhili wa serikali ya Marekani mkabala wa kusaini kile kinachojulikana kama   “Compact for Academic Excellence in Higher Education.”

Chuo Kikuu cha Arizona kimesema katika taarifa yake kwamba chuo hicho kinathibitisha kujitolea kwa uhuru wa kitaaluma, kwa tafiti zinazozingatia sifa na kwa uhuru wa kitaasisi na kueleza kuwa mapendekezo mengi  yamewasilishwa chuoni hapo na baadhi yake yanahitaji kuzingatiwa kwa makini. 

Hadi sasa Chuo Kikuu cha Brown, MIT, Chuo Kikuu cha Kusini mwa California, Chuo Kikuu cha Pennsylvania, Chuo Kikuu cha Virginia, na Chuo cha Dartmouth navyo pia vimepuuzilia mbali matakwa ya sera hiyo mpya ya Trump. 

Tangu kuanza kwa muhula wa pili wa uongozi wa Donald Trump mwezi Januari mwaka huu, serikali ya Marekani imepunguza mabilioni ya ufadhili wa masuala ya utafiti na kuhusisha suala la ruzuku na harakati za kisaisa za vyuo vikuu khususan vile vinavyoandaa maandamano ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina Wapalestina au kusaidia uendesaji wa programu mbalimbali. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *