
Haya yanajiri siku chache kabla ya Korea Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia-Pasifiki, APEC.
Mkutano huo utafanyika wiki ijayo katika mji wa Gyeonju na kuhudhuriwa na marais Donald Trump wa Marekani na yule wa China Xi Jinping pamoja na viongozi wengine wa ulimwengu.
Awali wataalamu walisema Korea Kaskazini inaweza kufanya majaribio ya uchochezi kwa kufyetua kombora kabla au wakati wa mkutano huo wa kilele wa APEC ili kusisitiza azma ya nchi hiyo kutambulika kama taifa lenye silaha za nyuklia.