
Donald Trump amesema hataki “mkutano wa kupoteza muda” baada ya mpango wa mazungumzo ya ana kwa ana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kuhusu vita vya Ukraine kuahirishwa.
Rais Trump amedokeza kuwa kukataa kwa Urusi kusitisha vita katika maeneo ya mipaka na Ukraine ndilo suala tete linalofanya mazungumzo kuwa magumu kufanyika.
Hapo awali, afisa wa Ikulu ya White House alisema “hakuna mipango” ya mkutano wa Trump-Putin “katika siku za usoni”, baada ya Trump kusema Alhamisi kwamba wawili hao watafanya mazungumzo huko Budapest ndani ya wiki mbili.
Tofauti kuu kati ya pendekezo la Marekani na Urusi kwa ajili ya amani ilizidi kuonekana wazi wiki hii, na kuonekana kupoteza nafasi ya mkutano wa kilele.
Uamuzi wa White House wa kuahirisha mipango ya mkutano wa pili wa Trump na Putin unaweza kuonekana kama jaribio la kuzuia hali nyingine kama hiyo.
“Nadhani Warusi walitaka sana na ikawa dhahiri kwa Wamarekani kwamba hakutakuwa na mpango wowote wa Trump huko Budapest,” mwanadiplomasia mkuu wa Ulaya aliiambia Reuters.
Hata hivyo,mjumbe maalum wa Urusi Kirill Dimitriev amesema matayarisho ya mkutano kati ya viongozi hao wawili yanaendelea.
Unaweza kusoma;